HabariMilele FmSwahili

Hoteli ya San-Valencia yafungwa kupitia amri ya serikali

Hoteli ya San-Valencia iliyoagizwa kufungwa na serikali imeridhia amri. Ujumbe uliopachikwa katika lango kuu la hoteli hiyo umeashiria hoteli hiyo itasailia kufungwa kwa muda usiojulikana. Ni hatua uongozi wa hoteli hiyo imechukua baada ya kuhusishwa na kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu hapa Nairobi. Wakati huo hoteli ya Jacaranda iliyofaa kufungwa pamoja na San-Valencia imekosa kutii amri, waziri wa afya kaunti ya Nairobi Bernard Muia akiahidi hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Show More

Related Articles