HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta na naibu wake wahudhuria mazishi ya mwendazake Biwott

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto ni miongoni mwa viongozi wa serikali wanaohudhuria hafla ya mazishi ya aliyekua waziri wa zamani Nicholas Biwott. Hafla hiyo inaendelea katika shule ya upili ya Maria Soti huko Keiyo Kusini kaunti ya Elgeyo Marakwet. Baadhi ya viongozi ambao tayari wamezungumza wakiwemo waziri wa zamani Henry Kosgei na makatibu wa wizara tofauti wamemtaja marehemu Biwott kama kiongozi aliyejitolea kuwahudumia wakenya katika nyadhfa tofauti. Biwott anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake katika kijiji cha Toot alasiri ya leo. Biwott alifariki wiki jana akiwa na miaka 78 baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Show More

Related Articles