HabariMilele FmSwahili

Mgombea kiti cha ubunge Rangwe Ezra Odhiambo hajulikani aliko

Polisi wameanzisha msako wa mgombea kiti cha ubunge eneo la Rangwe ambaye hajulikani aliko. Ezra Odhiambo mgombea wa chama cha Green Congress of Kenya alitoweka wikendi iliyopita huku jamii zake na marafiki wakiwa hawajui aliko. Wafuasi wa mgombea huyo wamekuwa wakishinikiza polisi kuimarisha msako wakidai huenda Odhiambo ametekwa nyara. OCPD wa Homabay Esau Ochorokodi anasema simu yake inaendelea kufanya kazi na wameanzisha harakati za kubaini iliko. Amewaonya wafuasi wake dhidi ya kueneza uvumi kuwa ametekwa nyara.

Show More

Related Articles