HabariMilele FmSwahili

Kampuni ya Al ghurair kuendelea kuchapisha karatasi za kura ya urais

Kampuni ya Al ghurair ya Dubai itaendelea kuchapisha karatasi za kura ya urais. Hii ni baada ya mahakama ya rufaa kuipa ushindi IEBC iliyowasilisha rufaa mahakamani kupinga uamuzi wa kubatilishwa kandarasi hiyo. Kwenye uamuzi wao majaji wa Erastus Githinji, Roselyn Nambuye, Alnasir Visram, Jamilla Muhammed na Otieno Odek wanasema mahakama kuu iliobatilia uamuzi huo ilikosea kwa kutozingatia muda uliosalia kabla ya uchaguzi. Jaji Githinji pia anasema mahakama kuu ilikosoea kwa kusema mazungumzo ya utoaji kandarasi hiyo ilifaa kufanyika kwanza na kuhusisha wakenya. Wakili wa IEBC Karuri Kamau amepongeza uamuzi huo akisema sasa IEBC itaweza kuendelea na mipango yake ya uchaguzi mkuu.

 

Show More

Related Articles