HabariMilele FmSwahili

Mkutano kati ya muungano wa wauguzi na baraza la magavana watibuka

Mkutano kati ya maafisa wa Muungano wa wauguzi na baraza la magavana umetibuka baada ya maafisa wa wauguzi kuondoka ghafla mkutanoni. Maafisa hao wakiongozwa na kaimu katibu Maurice Opetu na mwenyekiti Joseph Ngwasi hata hivyo hawakuweka Bayana sababu za kuondoka mkutanoni. Aidha baraza la magavana halijatoa tamko kuhusu hatua hiyo. Mkutano huo ulioandaliwa hapa Nairobi uliotarajiwa kuangazia lalama za wauguzi wanaogoma kuhusiana na utekelezaji mkataba wao.

Show More

Related Articles