HabariMilele FmSwahili

Vincent Onyango aapishwa kuhudumu kama afisa mkuu mtendaji katika idara ya polisi

Joseph Vincent Onyango ameapishwa rasmi kuhudumu kama afisa mkuu mtendaji katika idara ya polisi. Onyango anachukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa naye Ojango Omumu. Akiongea baada ya kuapishwa kwake Onyango ameelezea kujitolea kuhudumia wakenya idara ya polisi na serikali ya kenya.
Naye jaji mkuu David Maraga aliyeshuhudia kuapishwa kwake ametoa wito kwa tume ya huduma za polisi kukabili kwa usawa polisi wanaokiuka maadili. Amelalamikia uchunguzi duni unaofanyw ana polisi kwenye kesi zinazowasilishwa kotini.

Show More

Related Articles