HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta autuhumu upinzani kwa kuzua rabsha

Upinzani unanuia kuzua rabsha nchini kwa kuingilia utenda kazi wa idara ya usalama. Ndio usemi wa rais Kenyatta alipokutana na ujumbe wa muungano wa Afrika. Rais Kenyatta pia ametaja hulka ya upinzani kushutumu IEBC kila mara kama ishara ya kutokuwa tayari kwa uchaguzi huru. Katika mkao huo ulioongozwa na rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki na mwenyekiti wa muungano wa afrika Moussa Faki, Rais Kenyatta anasema upinzani umekataa kutangaza hadharani iwapo utakubali matokeo ya uchaguzi na hivyo kuzua tumbo joto miongoni mwa wakenya. Hata hivyo rais anasema mikakati imewekwa kuhakisha amani huku akirejelea ahadi yake ya kukubali matokeo.

Show More

Related Articles