HabariMilele FmSwahili

Kidero na Sonko wangepata asilimia sawa ya kura uchaguzi ungefanywa leo

Gavana Dkt Evans Kidero na mpinazni wake mkuu seneta Mike Sonko wangepata asilimia sawa ya kura iwapo uchaguzi ungeandaliwa leo. Kulingana na utafiti uliofanywa na shirika la TIFA gavana Kidero na seneta Sonko wana asilimia 41 ya umaarufu huku wawaniaji wengine wa kiti hicho Peter Kenneth na Miguna Miguna wakiwa na chini ya asilimia tano ya umaarufu. Hata hivyo asilimia saba ya wakazi wa Nairobi hawajaamua watakayemchagua. Katika kinyanganyiro cha useneta utafiti huo umemweka kifua mbele Johnson Sakaja wa Jubilee kwa asilimia 40 Edwin Sifuna wa ODM akifuatia kwa asilimia 24. Esther Pasari ni muaniji maarufu zaidi wa kiti cha mwakilishi wa kina mama huku Rechel Shebesh akifuatia kwa asilimia 31, asilimia 33 wakiwa hawajaamua wanayemuunga mkono.

Show More

Related Articles