HabariMilele FmSwahili

Serikali yaanza oparesheni ya kuwapokonya wakaazi wanaomiliki silaha kinyume cha sheria Kitui

Serikali imeanzisha oparesheni ya kuwapokonya bunduki wakazi wanaomiliki silaha kinyume cha sheria katika eneo la Mutomo huko Kitui. Kaunti kamishena Boaz Cherutich amewataka maafisa wa polisi kuwakamata watakaopatikana na silaha hizo. Cherutich pia amezindua operesheni ya kuifukuza jamii ya wafugaji wanaotoka kaunti ya Tana River kutoka mbuga ya wanyama pori huko Kitui kusini ili kusaidia kuregesha amani katika kaunti hiyo. Hii ni kufuatia msururu wa visa vya uvamizi wa wenyeji vinavyodaiwa kutekelezwa na wafugaji hao.

Show More

Related Articles