HabariMilele FmSwahili

Mahakama kutoa mwelekeo kuhusu kesi ya uchapizaji wa karatasi za urais leo

Majaji wa mahakama ya rufaa Erastus Githinji, Alnashir Visram, Roselyne Nambuye, Jamila Mohammed na Prof. James Odek Otieno wanaangaziwa zaidi leo wakitarajiwa kutoa mwelekeo kuhusiana na kesi inayopinga uamuzi wa kubatilisha kandarasi ya Al Ghurair ya kuchapisha karatasi za urais. IEBC wakili wa IEBC Kamau Karori alisema kampuni hiyo inafaa kuruhusuiwa kuendelea na zoezi la uchapishaji karatasi hizo kwani hakuna muda wa kutosha kutoa upya kandarasi nyingine. Mwanasheria mkuu Githu Muigai aliunga mkono kauli hii akisema huenda uchaguzi ukahujumiwa kwani majaji wakliopokonya alghurair kandarasi hiyo, walipuuza muda uliosalia kabla ya kuandaliwa uamuzi wao.

Show More

Related Articles