HabariPilipili FmPilipili FM News

Viongozi Wa ODM Klifi Waisuta Serikali Kuu.

Huku zikiwa zimesalia siku 19 tu wakenya waelekee kwenye debe viongozi wa kisiasa wanaogombea viti mbali mbali Kaunti ya Kilifi kwa tiketi ya chama cha ODM wameilaumu serikali ya Jubilee kwa kile wanachodai kuwa  wanatumia chakula cha msada kuwafanyia kampeni wagombea wao.

Akizungumza mjini Kilifi kwa niaba ya  viongozi hao gavana wa Kaunti hiyo Amason Kingi amesema kuwa ni haki ya wakazi hao kusaidiwa kwa chakula kwa sababu Kaunti hiyo ni miongoni mwa Kaunti zilizoathirika pakubwa na baa la njaa hapa nchini.

Show More

Related Articles