HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Watu 101 wameathiriwa na Kipindupindu Nairobi

Hoteli za Jacaranda na San Valencia jijini Nairobi zimeagizwa kusitisha utoaji huduma na wizara ya afya katika mojawapo ya hatua za kuthibiti mkurupuko wa ugonjwa wa Kipindupindu.
Hoteli hizo mbili zimefungwa baada ya kukosa kuafikia viwango vya wizara ya afya vinavyohusu uuzaji wa chakula.
Haya yanajiri huku idadi ya watu walioathiriwa na Kipindupindu ikifikia watu 101 hapa Nairobi ambapo 67 wamelazwa katika hospitali ya Nairobi.
Kulingana na waziri wa afya Cleophas Mailu ,serikali imeweka vituo saba nchini vya kuhudumia wagonjwa wa Kipindupindu.
Kama anavyotueleza Nancy Onyancha huenda ikachukua serikali juhudi za ziada kupambana na ugonjwa huu kwani wakenya wengi kwa kawaida huwa hawazingatii desturi ya usafi katika maeneo wanamokula au kunywa.

Show More

Related Articles