HabariMilele FmSwahili

Peter Kenneth aahidi kupunguza gharama ya kufanyia biashara Nairobi akichaguliwa

Mgombea huru wa ugavana Nairobi Peter Kenneth ameahidi kupunguza gharama ya kufanya biashara hapa Nairobi endapo atachaguliwa. Kenneth anasema ada wanaoyotozzwa wafanyibiashara wadogo wadogo itapunguzwa kutoka shilingi elfu 18 za sasa hadi elfu tano chini ya utawala wake. Akizungumza alipopeleka kampeini za kisiasa mtaani Zimmerman na Roysambu hapa Nairobi, Kenneth pia ameahidi kuekeza zaidi katika kujenga maeneo ya kuendesha biashara ili kutoa nafasi kwa vijana kupata ajira.

Show More

Related Articles