HabariMilele FmSwahili

Wauguzi Mombasa wamshtumu Joho kwa kulinyamazia swala la mgomo wao

Wauguzi kaunti ya Mombasa wamemshtumu gavana Ali Hassan Joho kwa kulinyamazia swala la mgomo wa wahudumu hao unaoendelea kwa zaidi ya mwezi sasa. Wakizungumza walipokuwa wameandamana mapema leo wauguzi hao wakiongozwa na katibu mkuu wa muungano wa wauguzi kaunti ya Mombasa Peter Maroko wamesistiza kuwa hawatorudi kazini hadi pale matakwa yao yatakaposikilizwa. Wamemtaka gavana Joho kuungana na wenzake katika kuhakikisha mkataba wao umetiwa sahihi.

Show More

Related Articles