HabariMilele FmSwahili

Jubilee yawarai wenyeji wa Pwani kuwachagua tena

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wamewarai wenyeji wa Pwani kuwachagua kuliongoza taifa kwa muhula wa pili. Wakihutubia mikutano ya kisiasa huko Changamwe kaunti ya Mombasa na Rabai kaunti ya Kilifi,rais na naibu wake wamesifia miradi iliokamilishwa na Jubilee miaka minne iliopita wakisema imebadili maisha ya wakenya. Viongozi hao ambao wamewahutubia wenyeji wa Taveta kaunti ya Taita Taveta,wameutaka upinzani kukoma kuingilia utenda kazi wa maafisa wa serikali badala yake kuangazia kuuza sera zao kwa wakenya. Rais na naibu wake wameelekea mjini Wundanyi kuhutubia mkutano wa kisiasa kabla ya kukamilisha ziara yao ya siku nne huko Pwani kwa kuwahutubia wananchi wa Mwatate na Voi mtawalia.

Show More

Related Articles