HabariMilele FmSwahili

NASA yaapa kulinda kura zao kuhakikisha hakuna visa vya wizi

Vigogo wa NASA wameapa kulinda kura zao siku ya uchaguzi kuhakikisha hakuna visa vyovyote vya wizi. Wakiwahutubia wenyeji wa Samburu,mgombea urais wa NASA Raila Odinga na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wanasema wana idadi ya kutosha ya kura kuwapa ushindi hivyo hatakubali yeyote kuhitilafyana na kura zao. Vinara hao ambao awali walikutana na mwenyekiti wa tume ya AU Mohammed Faki wamesema wanataka uchaguzi wa amani Agosti nane. Aidha vinara wenza wa NASA Musalia Mudavadi na Moses Wetangula wameilaumu serikali kwa kudinda kuitekeleza ripoti ya TJRC. Wakiongea eneo la Bukembe kaunti ya Bungoma,wamehaidi NASA itatekeleza ripoti hiyo kikamilifu iwapo watapata uongozi kuhakikisha waathiriwa wanapata haki. Kesho wana nasa watakua Kitui

Show More

Related Articles