HabariMilele FmSwahili

NASA yasisitiza kutekeleza ripoti ya TJRC iwapo watachaguliwa Agosti 8

Muungano wa NASA unasisitiza utaitekeleza kikamilifu ripoti ya TJRC iwapo utaunda serikali mwezi Agosti. Kinara wa ANC Musalia Mudavadi ameilaumu serikali kwa kupendekeza ripoti hiyo kufutiliwa mbali akisema hatua hiyo itawanyima waathiriwa haki. Akiwahutubia wenyeji wa Bukembe kaunti ya Bungoma kwenye ziara ya kujipigia debe, Mudavadi amewaomba wafuasi wao kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura siku ya uchaguzi akisema watatatua changamoto zinazowakabili. Wakati huo huo mgombea urais wa NASA Raila Odinga na mgombea mwenza wake kalonzo musyoka wameelekea kaunti ya Samburu ambapo wameratibiwa kuhutubia mikutano ya kisiasa mjini Maralal na Samburu.

Show More

Related Articles