HabariMilele FmSwahili

Makondakta 3 kunyogwa kwa dhuluma ya kijinsia Nairobi, Mahakama yaamuru

Wanaume watatu wamehukumiwa kunyongwa baada ya kupatikana na hatia ya kumpora kwa kutumia mabavu abiria wa kike mtaani Githurai maiaka mitatu iliyopita. Tatu hao dereva wa matatu ya kampuni ya Nazigi Sacco Edward Gitau, makanga Nicholas Mwangi na mhudumu katika kituo cha petroli cha Millenium Meshack Mwangi pia wamehukumiwa kifungo cha miaka 25 gerezani kwa kosa la kumdhulumu kimapenzi abiria huyo ndani ya matatu hiyo mnamo tarehe 19 septemba mwaka 2014. Akitoa hukumu dhidi yao hakimu mkaazi Francis Andayi amesema upande wa mashitaka umedhibitisha mashitaka dhidi yao. Pia amesema video iliyowasilishwa mahakamani kama ushahidi imedhibitisha kuwa walimdhulumu abiria huyo.

Show More

Related Articles