HabariMilele FmSwahili

Hoteli za Jacaranda na San Valencia zafungwa

Wizara ya afya imefunga hoteli za Jacaranda na San Valencia hapa jijini Nairobi kufuatia mkurupuko wa kipindupindu. Waziri Cleopa Mailu pia ametoa onyo kwa wamiliki hoteli kuwahawataruhusiwa kuagiza vyakula kutoka nje wanapokuwa na wageni. Mailu ametangaza kuwa wapishi wote katika hoteli watachunguzwa kikamilifu kabla ya kupata idhini ya kuhudumu. Ametaka wakazi kuzingatia usafi na kujiepusha wa kibinafsi ikiwemo kusafisha vyakula na mikono kabla ya kula ili kuepuka kuathirika.

Show More

Related Articles