HabariMilele FmSwahili

Ombudsman yaonya wanaotumia raslimali za umma katika kampeni za kisiasa

Tume ya haki maarufu Ombudsman, inawaonya wanaotumia raslimali za umma kuendesha kampeini za kisiasa. Mwenyekiti Dkt Regina Mwatha anasema tume yake inafuatilia kwa karibu kampeini zinazoendelea ili kuwachukulia hatua watakaopatikana. Ametoa onyo kali pia kwa maafisa wa serikali za taifa na wale wa kaunti dhidi ya kutumia mamlaka zao kuendesha kampeini, kwani ni hatia. Tayari tume hiyo imependekeza kuchunguzwa magavana watano akiwemo, Hassan Joho wa Mombasa, Paul Chepkwony wa Kericho, Peter Munya wa Meru, Simon Kachapin wa Pokot Magharibi na Julius Malombe wa Kitui kuhusiana na tuhma za kutumia raslimali za umma. Pia imependekeza kuchunugzwa makatibu Karanja Kibicho wa usalama na Patrick Njoroge wa kawi.

Show More

Related Articles