HabariMilele FmSwahili

Shehena ya kwanza ya karatasi za kupigia kura yawasili nchini

Shehena ya kwanza ya karatasi za kura zitakazotumika katika uchaguzi mkuu ujao zimewasili nchini. Karatasi hizo zilizowasilishwa nchini na kampuni ya Dubai ya Al Ghurair ni zile za uchaguzi wa magavana. Afisa mkuu wa tume ya uchaguzi IEBC Ezra Chiloba amesema karatasi za uchaguzi wa maseneta na wawakilishi wadi zitawasilishwa nchini wiki hii. Naye naibu mwenyekiti wa IEBC Consolata Nkatha amedhibitisha kuwa karatasi za kura ya wabunge zitawasilishwa nchini mwezi ujao. Hayo yanajiri huku mahakama ya rufaa ikitarajiwa kutoa uamuzi uamuzi wa mahakama kuu kuzuia kampuni ya Al Ghurai kuchapisha karatasi za kura ya urais.

Show More

Related Articles