HabariMilele FmSwahili

Waziri Mailu asisitiza mgomo wa wauguzi unaoendelea si halali

Waziri wa afya Dkt. Cleopa Mailu ameshikilia mgomo wa wauguzi ambao unaoendelea sio halali huku akiwataka kuusitisha. Akizungumza katika afisi ya kaunti kamishena wa Machakos, waziri Mailu amedokeza wauguzi hao walikiuka makubaliano waliyoafikia na serikali kuu wakati wa mgomo uliopita, hivyo KNUN wangewasilisha kesi mahakamani iwapo serikali imekiuka mkataba huo badala ya kufanya mgomo mwingine. Aidha amefedheheshwa na kufeli kwa makubaliano kati ya muungano wa wauguzi na ule wa magavana, wakiwataka kuwajali wananchi wanaozidi na kufa kwa kukosa matibabu.

Show More

Related Articles