HabariMilele FmSwahili

Jubilee kumaliza uskwota iwapo watachaguliwa kwa muhula wa pili

Serikali ya Jubilee itamaliza uskwota katika muhula wake wa pili wa uongozi. Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wanasema watahakikisha wakenya wote wanapata hati miliki za mashamba yao . Wakiongea huko pwani kwenye ziara ya kujipigia debe,wamewashtumu wapinzani wao kwa kutaka uchaguzi uhairishwe wakiwataja kama wasio na ajenda yeyote kwa taifa. Wamewaomba wenyeji kujitokeza kwa wingi Agosti nane kuwachagua viongozi wao.

Show More

Related Articles