HabariMilele FmSwahili

NASA yapuuza onyo la kutotangaza matokeo ya uchaguzi kabla ya IEBC

Vigogo wa NASA wamepuzilia mbali onyo la kutotangaza matokeo ya uchaguzi kabla ya IEBC . Akiongea kwenye ziara ya kujipigia debe Kibra Nairobi, kinara wa NASA Raila Odinga anasema mamlaka ya mawasiliano haina uwezo wa kutoa agizo hilo. Raila na mgombea mwenza Kalonzo Musyoka wamezionya idara huru dhidi ya kutumika kuhitilafyana na uchaguzi wakisema hawatakubali hatua hiyo kamwe. Aidha wana NASA wameilaumu serikali kwa kile wanadai kutowakabili watu fisadi.

Show More

Related Articles