HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Idara ya polisi yakanusha kuwepo shambulizi usiku wa manane

Afisa msimamizi wa oparesheni dhidi ya ugaidi katika msitu wa Boni amekanusha taarifa kwamba kulikuwepo mashambulizi makali baina ya polisi na wanamgambo wa Al-shabab katika kambi ya Mukowe, kaunti ya Lamu asubuhi ya kuamkia leo.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari,afisa huyo James Ole Serian, amesema milio ya risasi iliyosikika majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo ilitokana na hatua ya afisa mmoja aliyekuwa akishika doria kudhania kuwepo kwa shambulizi.
Haya yanajiri siku moja tu baada ya rais Uhuru Kenyatta kutoa onyo kali kwa wenyeji wa eneo la Pwani dhidi ya kuwalinda wafuasi wa kundi hilo la kigaidi.

Show More

Related Articles