HabariMilele FmSwahili

Wahadhiri wa vyuo vikuu wasitisha mgomo wao

Wahadhiri na wafanyikazi wa vyuo vikuu wamesitisha mgomo wao wa zaidi ya majuma mawili. Hii ni baada ya serikali ya kitaifa kukubali kutoa shilingi bilioni 5.2 zilizosalia kufanikisha mkataba wao wa bilioni 10. Wakiongea baada ya mazungumzo na upande wa serikali viongozi wa muungano wa UASU na KUDHEA wanasema kuwa serikali imetoa ahadi mpya za kufanikisha mkataba wao wa mwaka wa 2013 kufikia mwishoni mwa mwezi huu wa Julai. Serikali imetoa hakikisho kuwa mishahara ya wahadhiri na wafanyikazi wa vyuo vikuu ya mwezi huu itakuwa na mabadiliko hayo. Serikali pia imeonyesha nia ya kukamilisha mkataka wa mwaka wa 2017 na 2021.

Show More

Related Articles