HabariMilele FmSwahili

Elizabeth Ongoro asema maisha yake yamo hatarini

Seneta mteule Elizabeth Ongoro anasema kuwa maisha yake yamo hatarini. Akiwa mbele ya kamati ya nidhamu ya IEBC Ongoro anadai kuwa katika muda wa juma moja lililopita amekuwa akivamiwa na makundi ya wahuni wanakodiwa na wapinzani wake . Ongoro sasa analaumu tume hiyo kwa kukosa kuchukua hatua zozote dhidi ya wahusika licha ya kuiandikia barua mara saba kuhusu lalama hizo. Ongoro amefika mbele ya kamati hiyo baada ya mgombea wa Ruaraka Allan Juma kumlaumu Ongoro na mbunge Kajwang kwa kuondoa mabango ya matangazo yake.

Show More

Related Articles