HabariMilele FmSwahili

NASA kupeleka kampeini zake eneo la Kibra

Mgombea urais wa NASA Raila Odinga anatarajiwa wakati alasiri hii kuongoza mkutano wa kisiasa katika eneo la Kibra hapa Nairobi. Raila ambaye awali amehudhuria ibada ya wafu ya aliyekua waziri Nicholas Biwott anatarajiwa kuandamana na wanasiasa wanaowania nyadhfa tofauti kupitia muungano wa NASA hapa Nairobi. Aidha kinara wa ANC Musalia Mudavadi anaongoza mkutano sawia na huo kaunti ya Kakamega. Mudavadi akiandamana na wanasiasa wa NASA kaunti hiyo watahutubia mikutano kadhaa kaunti hiyo.

Show More

Related Articles