HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta awarai wenyeji wa Kwale kutogawanyika kwa misingi ya kikabila

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wamewarai wenyeji wa Kwale kutokubali kugawanywa kwa misingi ya kikabila taifa linapojiandaa kwa uchaguzi. Wakiwahutubia wenyeji wa Ukunda,rais na naibu wake wamesema taifa hili halifai kurejelea yalioshuhudiwa mwaka 2007/8 ili kuwanufaisha watu wachache wanaojitakia makuu. Wamesema kinyume na wapinzani wao wanaoeneza siasa za propaganda, lengo na Jubilee ni kuwaunganisha wakenya wote.
Huku wakisifia utenda kazi wa serikali yao,viongozi hao wamewaomba wenyeji kuwaunga mkono Agosti nane ili kuliongoza taifa kwa muhula wa pili.

Show More

Related Articles