HabariMilele FmSwahili

Kaunti ya Makueni yakanusha madai ya kuwepo ugonjwa wa kipindupindu

Serikali ya kaunti ya Makueni imekanusha madai ya kuwepo mkurupuko wa ugonjwa wa kipindu pindu katika kaunti hiyo. Waziri wa afya kaunti hiyo Andrew Mulwa anasema wameweka mikakati ya kuzuia uwezekano wa kutokea kwa visa vya ugonjwa huo. Akiongea katika kaunti jirani ya Machakos waziri wa afya Dkt. Cleopa Mailu amedokeza kwamba serikali ya kitaifa imeweka mikakati dhabiti kuhakikisha kwamba ugonjwa wa kipindupindu ambao umechipuka kwenye kaunti ya Nairobi hautoenea kwenye kaunti zingine.

Show More

Related Articles