HabariMilele FmSwahili

Waziri Mailu aagiza wapishi katika hoteli na mikahawa kufanyiwa uchunguzi

Waziri wa afya Cleopa Mailu ameagiza wapishi wote wanaohudumu katika Hoteli na Mikahawa kufanyiwa uchunguzi wa matibabu kufuatia mkurupuko wa kipindupindi kaunti ya Nairobi. Mailu amesema hatua hii inanuiwa kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huoambao tayari umesababisha vifo vya watu watatu. Akizungumza katika kaunti ya Kitui, Mailu pia amesema wachuuzi wa vyakula na maji hawataruhusiwa kuendeleza biashara zao.

Show More

Related Articles