BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Siegemei Mrengo Wowote Wa Kisiasa, Asema Willy Paul.

Msanii tajika wa nyimbo za injili nchini Willy Paul almaarufu Willy Pozee amepinga madai yakuegemea upande mmoja kwenye maswala ya kisiasa.

Ameyasema haya wakati wa mahojiano na kipindi cha Mwake Mwake Live na Gates Mgenge mjini Mombasa.

Willy Paul ambaye amekua akionekana kwenye mikutano ya kisiasa ya mrengo wa upinzani wa NASA hususani katika kaunti ya Mombasa ambako anaaminika kukita kambi amejitokeza wazi akisema yeye lengo lake kubwa kama msanii na kioo cha jamii nikuhubiri amani na wala sio kuegemea upande wowote wakisiasa.

“Mimi kwa sasa natumia taaluma yangu na kipaji changu kuhubiri amani wakati huu wa kampeni za kisiasa na kuonekana kwa mikutano ya kisiasa hio haimanishi ninaunga mkono upande mmoja apana mimi ni binadamu na lazma nilipe bills so natumia kipaji changu kuingiza hela”. Amesema Willy.

Wakati huohuo msanii huyo anayetamba na vibao vya Pilipili na Digirii ameweka wazi kuwa atakua kwenye tamasha kubwa litakalokuwa Nairobi wikendi hii ambapo msanii nguli kutoka Nigeria Wizkid atatumbuiza watu jijini. Nairobi

Show More

Related Articles