HabariPilipili FmPilipili FM News

Mkurugenzi Wa Mashtaka Ya Umma Akata Rufaa Dhidi Ya Kuachiliwa Kwa Wabakaji Mombasa.

Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma nchini amekata rufaa dhidi ya huku ya iliyotolewa na  mahakama mjini Mombasa yakuwaondolea mashtaka ya ubakaji jamaa watatu.

Jana mahakama mjini Mombasa iliwaondolea mashtaka ya ubakaji Jamal Salim, Mohamed Hassan na Daudi Mwachiro kwa kile hakimu Henry Nyakweba alichokitaja kuwa ushahidi uliowasilishwa mbele ya mahakama haukua na uzito huku akisema taarifa iliyoandikwa na mlalamishi ambaye alifariki kwa njia tatanishi kabla atoe ushahidi wake haungeweza kuzingatiwa kwa sana.

Hata hivyo afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma kupitia Eugene Wangila imekata rufaa dhidi ya uamuzi huo wakisema hakimu hakuzingatia swala lakuwa mlalamishi ni mtoto na alifariki kabla ya kutoa ushahidi ili hali uchunguzi wa madaktari ulionyesha mtoto huyo alilawitiwa.

Wakati huohuo Wangila amesema hakimu Nyakweba alijikanganya mwenyewe kwenye hukumu hiyo ikizingatiwa kuwa kulikua na taarifa ya marehemu iliyoandikwa na kuwasilishwa mahakamani.

Huku ametaka watatu hao wakamatwe na kuwa chini ya ulinzi hadi rufaa hiyo itakapo amuliwa.

Wakati wa hukumu yake hakimu Nyakweba aliilaumu afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma kwa kutofanya uchunguzi wa kina kuhusiana na kesi hio.

Fahimu Rashid alifariki kitatanishi kabla yakutoa ushahidi wake mahakamani dhidi ya washtakiwa.

Baada ya hukumu hio kutolewa Aisha Kalinga mama ya marehemu alizirai mahakamani  asiamini washtakiwa waliodaiwa kutekeleza unyama huo wako huru, watatu hao walikua wanakabiliwa na mashtaka ya kumlawiti kijana huyo wa umri wa miaka 13 kati ya tarehe 4 na 11 ya mwezi novemba  mwaka 2015

Show More

Related Articles