HabariPilipili FmPilipili FM News

Huduma Za Afya Zalemazwa Mombasa

Huduma za afya zinaendelea kuathirika katika hospitali nyingi za umma mjini Mombasa kufuatia mgomo wa wauguzi ambao unaingia wiki yake ya nne.

Akiongea na meza yetu ya habari mapema leo katibu mkuu wa chama cha wauguzi tawi la Mombasa Peter Maroko, ameonyesha wasiwasi wake kwamba maafisa wakuu serikalini wanaendelea na kampeni zao, badala ya kutafuta suluhu la kumaliza mgomo huo.

Maroko amesema hawana budi kuendelea na mgomo hadi serikali ikubali kuwalipa pesa zao, huku akizitaka serikali za kauti kushirikiana na serikali ya kitaifa kushughulikia suala hilo, kwani kwa sasa watu wengi wanaendelea kuathirika kutoakana na wao kukosa huduma muhimu za afya.

Show More

Related Articles