HabariPilipili FmPilipili FM News

Polisi Watibua Jaribio La Shambulizi La Al-Shaabab Mokoe.

Hali ya ati-ati imetanda kaunti ya Lamu baada ya watu wanaoaminika kuwa wanamgambo wa Alshabab kujaribu kuvamia kituo cha polisi eneo la Mokoe, usiku wa kuamkia leo.

Inaarifiwa tukio hilo limetokea majira ya saa saba usiku katika hali ambayo iliwalazimu maafisa wa polisi kufyatua risasi, baada ya watu hao waliokuwa katika makundi mawili kukosa kujitambulisha.

Akithibitisha kisa hicho kamishna wa kaunti ya lamu Joseph Kanyiri amesema kulikuwa na ufyatulianaji wa risasi karibu na kituo hicho na kwamba sio uvamizi kama inavyodaiwa.

Show More

Related Articles