HabariMilele FmSwahili

Waziri Keter aitaka IEBC kuhakikisha uchaguzi unafanyika kama ulivyoratibiwa

Waziri wa kawi Charles Keter ameitaka tume ya IEBC kuhakikisha uchaguzi mkuu unafanyika tarehe nane mwezi ujao jinsi ilivyoratibiwa kikatiba. Akihutubu kwenye uga wa Sosiot, kaunti ya Kericho, amekosoa uamuzi wa mahakama kuzuia uchapishaji wa karatasi za kupiga kura za urais. Keter kadhalika amesisitiza haja ya kampeni za amani huku akiwasihi wenyeji kumchagua Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kwa hawamu ya pili.

Show More

Related Articles