Elections 2017HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Vinara wawashinikiza wakazi kujitokeza kwa wingi Agosti 8

Vigogo wa muungano wa upinzani NASA hii leo walielekeza kampeni zao katika kaunti ya Homa Bay mojawepo ya ngome kuu za muungano huo kutokana na mtagusano wake kupitia chama cha chungwa , ODM.
Hata hivyo hii leo mkondo wa mambo ulikuwa tofauti kidogo kutokana na wana NASA kubadili mbinu waliyoitumia Nyamira ya kuinyoshea kidole cha lawama Jubilee na ujumbe wao uliangazia pakubwa ni vipi wafuasi wao watajitokeza kwa wingi Agosti tarehe nane na pia kulinda kura zao.
Anders Ihachi anazidi kufuatilia kampeni za NASA na anatujuza mengi kutoka Homa Bay ambapo pia mwenyekiti wa tume ya uiano, NCIC Francis Ole Kaparo amekashifiwa pakubwa kutokana na msimamo wake kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii.

Show More

Related Articles