HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wizara ya afya yafutilia mbali leseni zote za wauzaji vyakula

Wizara ya afya imefutilia mbali leseni zote za wachuuzi wa chakula katika hoteli na maeneo yote kunakouzwa chakula, na kuagiza maafisa wa afya katika kila kaunti kuhakikisha wamefanya uchunguzi upya na kutoa upya vyeti na leseni baada ya uchunguzi wa kina.
Hii ni kufuatia mkurupuko wa maradhi ya Kipindupindu haswa katika kaunti ya Nairobi, hali iliyopelekea vifo vya watu 3 kufikia sasa na mamia ya wengi kuuguzwa.

Show More

Related Articles