HabariPilipili FmPilipili FM News

Serikali Ya Kaunti Ya Kilifi Yapinga Kuajiri Wauguzi Wapya.

Idara ya afya kaunti ya Kilifi imekana madai kuwa ina njama ya kuajiri wauguzi wapya ili kufidia nafasi za wauguzi walioko katika mgomo.

Akipinga madai hayo afisa mkuu wa idara hiyo Timothy Malingi amesema kuwa zoezi hilo la kuajiri wauguzi hufanyika kila mwaka katika juhudi zao za kufanikisha huduma bora na wala sio kufidia nafasi za waliogoma.

Malingi amesema kuwa kauti hiyo kwa sasa ina wauguzi 530 pekee idadi ambayo ni haba mno kuhudumia wananchi.

Aidha afisa huyo amesema kuwa mgomo wa wauguzi unaoendelea umeathiri mno huduma za matibabu hasa katika hospitali kuu za kauti hiyo ikiwemo Kilifi, malindi na Maryakani.

Hata hivyo Malingi ameitaka wizara ya afya ya kitaifa pamoja na  tume husika kujaribu kutatua suala hilo kwa haraka wakati serikali ya kaunti nayo ikiendeleza mazungumzo na viongozi wa muungano wa wauguzi ili kuhakikisha matakwa yao yanatatuliwa na kurudi kazini.

 

Show More

Related Articles