HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakuu Wa Makundi Ya Mtandao Wa Watsapp Kujipata Pabaya.

Huenda wakuu wa makundi ya Watsup wakajipata mashakani iwapo mtu yeyote katika makundi hayo ataeneza jumbe za uchochezi.

Mwenyekiti wa tume ya uwiano na utangamano nchini NCIC Francis Ole Kaparo, anasema wote wanaounda makundi kwenye mitandao ya kijamii kama vile watsup wana jukumu la kithibiti semi za chuki, na iwapo watakosa kuzingatia hilo watalazimika kuchukuliwa hatua kali kisheria.

Anasema kufikia sasa wametambua jumla ya makundi 21 ya watsup katika kaunti mbalimbali nchini, ambayo yamekuwa yakitumiwa kueneza uchochezi baina ya jamii mbali mbali.

Nao muungano wa makanisa umeitaka tume ya uchaguzi nchini kujitahidi kuandaa uchaguzi huru na wa haki kuona kuwa hali ya utulivu inasalia imara kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

Show More

Related Articles