HabariMilele FmSwahili

Maandalizi ya mjadala wa kwanza wa wagombea wenza yakamilika

Maandalizi ya mjadala wa kwanza wa wagombea wenza nchini yamekamilika. Usalama umeimarishwa katika chuo kikuu cha Catholic viungani mwa jiji la Nairobi. Kwa mujibu wa waandalizi mjadala h uo uanatarajiwa kuanza saa 4.30 alasiri hii. Hata hivyo naibu wa rais William Ruto hatohudhuria mjadala huo na badala yake atashiriki kampeni za kuipigia debe Jubilee katika kaunti za Pwani. Naye Kalonzo Musyoka kufikia sasa haijabainika iwapo atahudhuri mjadala huo au la.

Show More

Related Articles