HabariMilele FmSwahili

Esipisu:Rais kuzuru kaunit 14 Juma moja lijalo kusaka kura kabla ya uchaguzi mkuu

Rais Uhuru Kenyatta atazuru kaunti 14 jumamoja lijalo kusaka kura kabla ya uchaguzi mkuu. Katika taarifa msemaji wa ikulu Manoah Esipisu amesema rais ambaye kwa sasa yuko kaunti ya Pwani anatarajiwa kuzuru kaunti za Lamu, Tanariver na Taita Taveta katika siku tatu zijazo. Baadaye ataelekea kaunti ya Elgeyo Marakwet kuhudhuria mazishi ya mwanasiasa mkongwe Nicholas Biwott. Rais Kenyatta pia ameratibiwa kuongoza kampeni za Jubilee Nairobi, kabla ya kuzuru Garisa, Mandera, Isiolo, Wajir na Samburu.

Show More

Related Articles