HabariMilele FmSwahili

Mrengo wa NASA wabuni kundi la usalama kuzuia wizi wa kura

Mrengo wa NASA umebuni kundi la usalama litakaloshika doria katika vituo vya kupigia kura kwa lengo la kuzuia wizi wa kura. Wakiongozwa na mgombea urais wa NASA Raila Odinga kwenye kampeni zao huko Nyamira wana NASA wanasema kila kituo kitakuwa na watu 5 watakaofuatilia zoezi hilo. Wakiongea kwenye ziara yao katika maeneo ya Magwanga Ikonge na Kebirigo wana NASA wanasisitiza kuwa wataendesha shughuli ya kuhesabu kura sambasamba na tume ya IEBC. Raila anasema lazima serikali ya Jubilee iondolewe afisini kwa kuwa imelemaza uchumi wa nchi. Raila anasema miradi mingi inayozinduliwa na Jubilee kwa sasa ikiwemo ujenzi wa barabara ilianzishwa wakati wa serikali yake na rais mustaafu Mwai Kibaki

Show More

Related Articles