HabariMilele FmSwahili

Ruto hatohudhuria mdahalo wa manaibu wa rais leo

Naibu wa rais William Ruto hatohudhuria mjadala wa manaibu wa rais uliopangiwa kufanyika hii leo katika chuo kikuu cha kanisa Katoliki mtaani Karen. Ruto ambaye atawakilishwa na mbunge wa Kikuyu Kimani Ichungwa kwenye mjadala huo anasema kuwa hataweza kuwepo kwa kuwa ataandamana na rais Kenyatta kwenye kampeni zao za kisiasa maeneo ya lamu na Tana River. Kwa upande wake ichungwa amesema kuwa yuko tayari kumwakilisha naibu wa rais kwenye mjadala huo japo kamati andalizi ya mjadala husika inasema huenda ikawa vigumu Ichungwa kuruhusiwa kumwakilisha Ruto. Jumla ya wagombea wenza nane wanatarajiwa kuyhudhuria mdahalo huo.

Show More

Related Articles