HabariMilele FmSwahili

Huenda wananchi wa Kitutu Chache Kusini kukosa kumchagua mbunge wao Agosti nane

Huenda wananchi wa eneo bunge la Kitutu Chache Kusini wakakosa kumchagua mbunge wao Agosti nane kufuatia kifo cha mmoja wa wagombea hapo jana. Hii ni baada ya mgombea ubunge Leonard Mwamba aliyekua anapeperusha bendera ya chama cha Jubilee kufariki katika ajali mbaya ya barabarani iliotokea barabara kuu ya Kisii-Kisumu katika kituo cha biashara cha nyakoe. Afisa wa mawasiliano wa tume ya uchaguzi IEBC Andrew Limo anasema uchaguzi huo utahairishwa hadi mgombea mwingine kuteuliwa kupeperusha bendera ya jubilee. Ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu wengine wawili akiwemo mwanafunzi wa shule ya msingi. Kamanda wa polisi mjini Kisii Hassa Abdi anasema uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Show More

Related Articles