HabariMilele FmSwahili

Wazee Bomet wakemea matamshi ya Isaac Ruto

Wazee kaunti ya Bomet wamekemea vikali matamshi ya gavana Isaac Ruto aliyotoa siku ya Alhamisi kutishia kuvuruga kampeni za Jubilee
kaunti hiyo. Wakiongozwa na Phillip Chebosir,wazee hao wanasema matammshi hayo yanaweza kuibua uhasama na hayakustahili kutolewa na kiongozi kama gavana Ruto. Wazee hao wamemlaumu gavana huyo kwa kutoa matamshi ya kuwadhalilisha kinamama huku wakimtaka kujiandaa kushindwa katika uchaguzi mkuu mwezi ujao. Gavana huyo alitishia kuwarai wafuasi wa chama chake cha mashinani kuvuruga mikutano ya rais Kenyatta na naibu wake William Ruto kaunti hiyo endapo viongozi wa upinzani hawatapokelewa vyema kwenye ngome za Jubilee.

Show More

Related Articles