HabariMilele FmSwahili

NASA kupeleka kampeini zake eneo la Kaskazini Mashariki

Muungano wa NASA leo unapeleka kampeni za kujipigia debe eneo la Kaskazini mashariki hii leo. Vigogo wa NASA wakiongozwa na mgombea urais Raila Odinga na mgombea mwenza Kalonzo Musyoka wanatarajiwa kuzuru miji ya Moyale,Marsabit na Laisamis kuwarai wenyeji kuwaunga mkono ifikiapo Agosti nane. Jana wana NASA walizuru maeneo kadhaa kaunti ya Nairobi ambapo waliwarai wenyeji kujitokeza kwa wingi Agosti nane kuwapigia kura. Yakijiri hayo,mbunge wa Matayos Geofrey Odanga amemtaka gavana wa  Busia Sospeter Ojaamong na seneta Amos wako kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kushirikiana kuhakikisha chama cha ODM kinanyakua viti vingi eneo hilo. Odanga amewataka viongozi na wawaniaji wote wa ODM kaunti hiyo kuungana kukitafutia uungwaji mkono chama hicho.

Show More

Related Articles