HabariMilele FmSwahili

Serikali yaahidi kuhakikisha masomo ya shule yanaingia katika mfumo wa dijitali

Serikali itaendelea na juhudi za kuhakikisha masomo ya shule za msingi na upili yanaingia katika mfumo wa dijitali kama njia mojawpao ya kutimiza ruwaza ya mwaka wa 2030. Katibu katika wizara hiyo Belio Kipsang anasema mafunzo hayo yatawawezesha wanafunzi kupata maarifa kuhusu masuala mbalimbali. Kwenye hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na mkurugenzi wa elimu ya msingi Paul Ronoh,katika shule ya Kaptebeswet,kaunti ya Kericho,katibu huyo amesisitiza haja ya ushirikiano miongoni mwa wadau wa sekta ya elimu kufanikisha lengo hilo.

Show More

Related Articles