HabariMilele FmSwahili

Daniel Moi: GG Kariuki alikua kiongozi wa kujitolea katika utendakazi wake kwa taifa

Seneta GG Kariuki alikua kiongozi alijitolea katika utenda kazi wake kwa taifa. Ndio ujumbe wa marais wastaafu Daniel moi na Mwai Kibaki katika risala zao kwenye hafla ya mazishi ya mwenda zake inayoendelea huko Rumuruti kaunti ya Laikipia. Kwenye risala zake kupitia seneta Gideon Moi, rais msaafu Moi amemtaja mwenda zake kama kiongozi aliyekua na mchango mkubwa katika serikali yake. Naye Kibaki kwenye risala zake kupitia Nderitu Mureithi amesifia mchango wa marehemu katika kuhakikisha usalama maeneo tofauti nchini.

Show More

Related Articles