HabariPilipili FmPilipili FM News

Shahabal Awasuta Wapinzani Wake.

Mwaniaji wa kiti cha ugavana kwa tiketi ya chama cha Jubilee Suleiman Shahbal amewataja wapinzani wake wa kisiasa kama wasio na sera za maendeleo baada ya wao kukosa kufika katika mdahalo uliondaliwa na muungano wa wazalishaji bidhaa hapa Mombasa Kenya association of manufactures

 

Shahbal ambaye amekua mgombea pekee kuhudhuria kikao hicho ameitaja hatua ya kukwepa kuhudhuria mjadala huo kwa wagombea Hassan Sarai wa chama cha Wiper, Hezron Awiti wa VDP na gavana wa Mombasa Hassan Joho kama kitendo cha uoga na kukosa ajenda za kuwaelezea wakaazi wa Mombasa kwa kukosa manifesto

Shahabal amewataja viongozi hao kuwa wanakosa sera za  kuinua uchumi wa kaunti ya Mombasa ambao umeonekana kuzorota kwa kipindi cha miaka minne .

Shahbal amewataka wakaazi wa Mombasa kuwachunguza viongozi na kuchagua wenye sera za maendeleo na wenye uwezo w a kushirikiana na wawekezaji ili kusaidia katika kubuni ajira na kukabiliana na umaskini

 

Show More

Related Articles